Challenge:

Khanga Design Challenge

MPE NAFASI MTOTO WA KIKE

Christina Lwendo


Title

MPE NAFASI MTOTO WA KIKE

Name: Artist/Group

Christine Lwendo

Describe your idea (200 Words)

Vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimekua vikiangaliwa kwa jicho la karibu zaidi hivi karibuni kutokana na muamko chanya unaoendelea kujitokeza katika jamii. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kwamba vitendo hivi vimezidi kukithiri katika baadhi ya maeneo ya Tanzania kuanzia mwaka 2010 (chanzo; BBC SWAHILI). Hivyo nimebuni khanga ambayo italeta ujumbe chanya katika jamii, si tu kwa kuwajulisha watu juu ya unyanyasaji, bali pia kutoa maoni nini kifanyike ili kuweza kupunguza na hatimaye kutokomeza kabisa tatizo hili. Khanga hii ina alama muhimu tatu ambazo zinabeba wazo kuu la 'MPE NAFASI MTOTO WA KIKE'. Alama ya kwanza ni machozi, hii inawakilisha kilio cha jinsia ya kike juu ya kunyanyasika na kutaka kusikilizwa na jamii inayowazunguka. Alama ya pili ni umoja wa jinsia ya kike kuungana ili kupaza sauti zao kwa umoja zaidi, jamii iweze kutilia mkazo jambo hili. Nadhani ni muhimu pia kwa waathirika wa matukio haya kuwa wajasiri, kujitokeza, kuungana na kusema hapana. Na alama ya tatu inaonyesha kwamba alama ya jinsia ya kike ni sawa na ile ya jinsia ya kiume. Hapa namaanisha kwamba jamii inapaswa kujua na kutilia maanani kwamba mtoto wa kike naye ni haki apewe thamani sawa na mtoto wa kiume. Pia ujumbe wa kanga usemao "Usiponikandamiza , umenitoa kwenye giza" unaihusia jamii kuwa mtoto wa kike anao uwezo wa kufanya mengi mazuri iwapo atapewa nafasi. Kutokumkandamiza kunamuwezesha yeye kufungua mabawa yake, kupaa, kustawi na kuimarika.

Khanga Tagline

USIPONIKANDAMIZA, UMENITOA KWENYE GIZA

Comments