Challenge:

Khanga Design Challenge

Mwili Wako Sio Duka.

EMMANUEL MARAHU


Title

Mwili Wako Sio Duka.

Name: Artist/Group

EMMANUEL MARAHU as CHUCHA DESIGNER

Describe your idea (200 Words)

Ujumbe wangu Mkuu katika hili shindano la Ubunifu wa Khanga katika kuzungumzia Elimu Ya Afya Ya Uzazi ndani ya wilaya ya Temeke ni swala la Biashara ya ngono inayofanyika kila siku katika mitaa ya Wahaya street around na Temeke hospital. Wadau wakuu ni Serikali yangu ya Tanzania na jamii yote ni kiwalenga wamiliki wa vibanda na vyumba vinavyokodishwa kwa Dada na Mama zetu kufanya biashara ya kuuza miili yao, hofu yangu ni kusambaa kwa magonjwa ya zinaa na gonjwa kuu la Ukimwi kwa vijana wanao penda kufika meeneo haya kununua miili ya Mabinti na akina Mama. Nimepata Data hizi kwa kufika eneo hili husika la Wahaya Street na kujionea biashara ya ngono ikiendelea kushika hatamu kila siku husuani kuanzia mida ya jioni. Nashauri Elimu itolewe kwa kuwaelimisha Mabinti na akina Mama kuachana na uuzaji miili yao na kujishughulisha na biashara ndogondogo au miradi ya kimaendeleo inayoweza kuwakwamua kiuchumi na kuwapatia kiapato.Pia nashauri Serikalai ichukue jukumu mara moja la kuwakamata wote wanaopangisha maeneo hayo na kuyafungia, kwani tayari yamepelekea Mmomonyoko wa kimaadili kwa Watoto na vijana wadogo wengine wakiiga tabia za Dada, Mama na Kaka zao amabao ndio wadau wa biashara hiyo. Hatua zikichukuliwa basi jamii na kizazi cha Wilaya Ya Temeke haitazidi kupotea maana ni watu tunaoishi nao kila siku na nimaisha ambayo si rasmi katika tamaduni za kitanzania na taratibu zake.

Khanga Tagline

NAWEZA BILA YAKO

Comments