Challenge:

Khanga Design Challenge

usinichoshe

jacob sebastian


Title

usinichoshe

Name: Artist/Group

jacob sebastian

Describe your idea (200 Words)

katika wilaya ya temeke ni moja kati ya sehemu zilizotajwa kuwa na matatizo mengi kuhusu ukosefu wa afya ya uzazi wa mpango yanayo wakabili raia wengi . Katika mchoro wangu umaonesha mama ambaye ameonekana kutofuata ama kutotumia uzazi Wwa mpango. Kama kichwa cha habari kinavyosema "Usinichoshe" Kwani ni muhimu kufahamu umuhimu wa afya ya nzuri kwa uzazi uliosalama kwani taifa la Leo likiokoka na majanga haya ya kupewa elimu kwa njia mbalimbali hasa hii ya khanga, itawasaidia kuepukana na tatizo la kutotumia njia ya uzazi wa mpango. Kwa mujibu wa data zilizokusanywa na uchunguzi uliofanikoshwa ni kwamba kinamama walio wengi wamekuwa wakitumia njia zisizo salama ambazo zinaweza kuwapelekea wakikumbwa na tatizo la uzazi. Ni wito kwa wazazi wote Kufahamu njia za uzazi wa mpango zilizosalama ili kuweza kuokoa taifa la kesho . Kwani kesho Tanzania iko mikononi mwa jamii nzima. Wananchi wa serikali inawajibu Kufahamu njia za uzazi wa mpango ni muhimu kwa afya ya mama na mtoto ili Iweze Kusaidia kupunguza idadi ya vifo kwa wamama wajawazito na watoto pia. Hata kuweza kumsaidia mama kupumzika na kuweza kufanya shughuli nyengine za kimaendeleo.

Khanga Tagline

tusipopanga uzazi tutaaribu malengo

Comments