Challenge:

Khanga Design Challenge

Kizazi huru

Paris Joseph


Title

Kizazi huru

Name: Artist/Group

Nancy Joseph

Describe your idea (200 Words)

Katika mpango wa maendeleo endelevu ya umoja wa taifa lile lengo la 3 linalenga kupunguza vifo vya watoto na kujenga jamii yenye afya.Swali kubwa ambalo nimekuwa nikijiuliza ni kwamba tunawezaje kujenga jamii yenye afya bila kuangalia afya ya mtu mmoja mmoja au jamii zinazotunguka. Nitatumia wilaya ya Temeke kama mfano wa jamii yenye vijana wengi wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya,hii hupelekea wengi wao kujikuta wakijihusisha na ngono zembe,maambukizi ya ukimwi kitu kinachohatarisha afya za mama na mtoto na pia malezi bora. Takwimu zinaonyesha kuwa 86.5% ya wanaume 1546 na 13.5% ya wanawake 241 ya idadi ya watu walio katika umri wa miaka 12-54 wamesajiliwa kutumia madawa ya kulevya katika hospital ya Muhimbili,Temeke na Mwananyamala (Chanzo:Wizara ya Afya na ustawi wa jamii),hii inamaanisha kuwa jamii hii ipo katika hatari kubwa ya kusambaa kwa Ukimwi, wazazi wasio na malezi bora kwa wototo na pia ubakaji au uhalifu wa kingono, hivyo basi ili kuweza kupata jamii bora katika wilaya ya Temeke, Tanzania na pia kufikia malengo ya umoja wa mataifa,kampeni yangu ya kizazi huru inalenga katika kuhamasisha,kuelimisha kuhusu madawa ya kulevya na elimu ya afya ya uzazi na pia kutumia njia bunifu ya kiburudani kuwawezesha vijana na wanawake kukimbia tabia hatarishi na kujenga jamii bora yenye mlengo bora kwa maendeleo ya taifa na dunia kwa ujumla.

Khanga Tagline

Maisha Yako,kesho yako

Comments