Challenge:

Khanga Design Challenge

NAKUHESHIMU ILA UNANIDHALILISHA VILIVYO

eric papian


Title

NAKUHESHIMU ILA UNANIDHALILISHA VILIVYO

Name: Artist/Group

Erick Papian

Describe your idea (200 Words)

Unyanyasaji wa kijinsia ndiyo nazungumzia, imekuwa changamoto kubwa katika taifa letu utafiti umefanyika Temeke na imegundulika kuwa kwa kiasi kikubwa wanawake wananyanyaswa kijisinsia na wanaume, imeshuhudiwa wakitukanwa na kupigwa bila sababu.Utafiti uliofanyika mwaka 2010 na TDHS (Tanzania Demographic Health Survey) unaonesha kuwa wanaume 4 kati ya 10 walikubali kuwa kupiga wake zao ni sawa , na siyo katika utafiti huu tu hata ukiangalia tafiti zingine zilizofanyika Temeke utagundua wanawake wananyanyaswa sana jambo linalosababisha wanawake kuwa wanyonge katika jamii, mfano mzuri ni familia yetu ambapo Baba alipomzuia mama kwenda kusoma akisema anastahili kukaa nyumani tu mama alipolazimisha alipigwa na kutukanwa hadhalani bila msaada wowote mama alijitahidi akaenda kusoma jambo ambalo lilimperekea kufukuzwa nyumbani na kusababisha mpasuko wa familia, hivyo unaweza kuona jinsi unyanyasaji huu unavyosababisha madhara makubwa.Nimeonyesha vizuri kwenye design yangu katika eneo la mji wa Kanga kuna ua lenye matawi 6 likiwakilisha wanawake 6 ndani yake wamewakilishwa wanawake 4 kwa rangi nyekundu kuonyesha kuwa kati ya wanawake 10 wanawake 4 wako hatarini kwa unyanyasaji wa kijinsia. hivyo napenda kushauri taasisi mbalimbali za uma na binafsi kuhakikisha elimu juu ya ukatili wa kijinsia inaifikia jamii ili kuhakikisha tatizo hili linatoweka kabisa katika jamii zetu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Khanga Tagline

HESHIMA HAIJI KWA KUNIDHALILISHA

Comments