Challenge:

Khanga Design Challenge

VIFO VYA MAMA NA MTOTO

ANNA BEN


Title

VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Name: Artist/Group

ANNA BEN

Describe your idea (200 Words)

Tunapoizungumzia Temeke tunazungumzia watu wanaoishi katika manispaa hiyo idadi kubwa ikiwa ni wanawake (51%)-chanzo ofisi ya serikali kitengo cha taarifa za afya 2016-2017.Licha ya kuwa na vituo vya afya 126 bado temeke inaangalia vifo vya mama na mtoto kama moja ya Changamoto kubwa vyanzo Vikubwa ni ukimwi kwa wanawake (52%) Watoto kuzaliwa njiti (33%) homa ya mapafu (29%) Na vifo baada ya kujifungua (4%).Mradi sanifu uitwao "Uokoaji wa wamama na Watoto " uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali (2016),ulibaini kuwa wanawake 24 na Watoto 49 Kati ya vizazi hai 1000 hupoteza maisha kila siku vyanzo Vikubwa vikiwa ni ukosefu wa dawa na vifaa, vyumba vya dharura, Mila potofu na elimu duni kwa wauguzi na wananchi. Katika ubunifu wangu Nimetumia Rangi ya kijani Inayosimamia uhai,nyekundu Inasimamia kifo, nyeusi na nyeupe kunogesha ubu/nifu wangu,ukumbi wa khanga una mchoro wa mama Na mtoto Ukimaanisha Mada niliyoichagua "vifo vya mama na mtoto" wakati huo kuna majani manne Kati ya hao matatu yana rangi Nyeupe na moja Lina rangi nyekundu kumaanisha Kati ya vizazi hai Vinne mama mmoja hufariki dunia wakati/baada ya kujifungua... Na katika mpaka wa khanga hii tunaona majani sita matano ya rangi ya kijani moja jekundu hii Ikimaanisha Kati ya Watoto sita wanaozaliwa mmoja anafariki wakati /baada ya kuzaliwa.Tokomeza vifo vya mama Na mtoto tufikie uchumi wa viwanda kwani Maendeleo yetu na ya taifa yanategemea afya zetu. "Chungu cha moto hiki Bila ufundi huipui" wakati unatumia chugu kupikia mboga, mboga ikiiva Unahitaji umakini wakati unakitoa changu jikoni... Ukikitoa vibaya kikidondoka lazima kitapasuka na mboga itamwagika. Chungu ni Mwanamke mtoto ni mboga tusipomuhudumia mama mjamzito vizuri wakati wa kujifungua tutapoteza maisha yake na ya mtoto pia.

Khanga Tagline

CHUNGU CHA MOTO HIKI BILA UFUNDI HUIPUI

Attachments

Comments