Challenge:

Khanga Design Challenge

Muhimu kuanza uzazi kwa wakati

Merina Massi


Title

Muhimu kuanza uzazi kwa wakati

Name: Artist/Group

Merina Massi

Describe your idea (200 Words)

Swala la mimba za utotoni limekuwa janga kubwa katika jamii yetu.Licha ya kuwepo kwa madhara kubeba mimba katika umri mdogo.Takwimu zinaonesha kila walipo mabinti wa umri kuanzia miaka 12-18 walipo mabinti kumi basi watatu kati yao ni wajawazito au wanawatoto. Ubebaji mimba katika umri mdogo unapelekea mama kupata matatizo wakati wa kujifungua matatizo hayo ni kama kutoka na damu nyingi wakati wa kujifungua, kupoteza maisha ya mama na mtoto hii inatokana na kuwa viungo vya binti huyu kuwa havija komaa. Mambo haya yanatoke katika jamii zetu.. yanawakumba wadogo zetu,mabinti zetu wa umri mdogo sana.Hivyo ni maswala yanayogusa familia zetu, maisha yetu na jamii kiujumla. Wito wangu kwa jamii, wanawake kwa wanaume kuhakikisha tunawalinda mabinti wa umri kati miaka 12-18 kuhakikisha tunawalinda kwa kuwawekea mazingira mazuri, mbali na vishawishi vya kujamiiana na kuwaondolea mazingira ambayo yanaweza kuwafanya kujiingiza katika vitendo vya kujamiiana katika umri mdogo. Hali hii itapunguza wimbi la mimba za utotoni na kupelekea kujenga taifa lenye vijana wenye nguvu na uelewa mkubwa kuhusiana na elimu ya kijinsia na jinsi ya kujitunza katika ujana wao.

Khanga Tagline

Kwa Chumvi Usinile

Comments