Challenge:

Khanga Design Challenge

Wema huanzia nyumbani/charity begins at home

zaitun rungwe


Title

Wema huanzia nyumbani/charity begins at home

Name: Artist/Group

Zaituni Rungwe

Describe your idea (200 Words)

Watu wakitaka kukujua zaidi huangalia jamii iliyokuzunguka,kuna msemo unaosema nionyeshe marafiki zako nitakuambia wewe ni nani,mimi nitaipeleka mbali zaidi kwa kusema nionyeshe jamii yako na nitakuambia wewe ni nani.Huwezi kuitwa Kiongozi bora kama jamii yako haina usawa,huwezi kuitwa mume au baba bora kama unamnyanyasa mke wako,huwezi kuitwa mama bora kama watoto wako hawana maadili na hatuwezi kuitwa nchi bora kama jamii yetu haitakua katika usawa kijinsia na pia kuendelea kiuchumi.Mara nyingi ninapomtazama Mwanamke naiona sura na kesho ya taifa,hii ni kwa sababu mama ni mwalimu wa kwanza kwenye jamii.Kwa muda mrefu sana jamii yetu imekuwa ikisumbuliwa na tatizo la ukatili wa kijinsia hali ambayo jinsia moja inainyima haki ya msingi jinsia nyingine,ukatili huu ambao upo katika hali ya kimabavu,kingono (ubakaji),kisaikolojia na kiuchumi(rushwa ya ngono).Takwimu zinaonyesha kuwa msichana mmoja kati ya 5 hukatiliwa kimabavu au kingono duniani.Katika wilaya ya Temeke wanawake 5463 ambao ni sawa na 79% ya wahanga waliofika katika dawati la jinsia wamenyanyaswa kijinsia na pia wanaume 1426 ambao ni sawa na 21%,hali hii huatarisha afya ya wahanga na taifa kwa ujumla sababu ya kuwaweka wahanga katika hatari ya kupata maambukizi ya ukimwi,kuharibu njia za uzazi hasa ubakaji na uingiliwaji wa kinyume na maumbile lakini pia mhanga kupitia hali ya kuathirika kisaikolojia hivyo kushindwa kufurahia maisha na kufanya kazi kwa ufanishi hivyo basi kupelekea taifa kuwa katika hatari kiuchumi,kiafya na pia kijamii. Ikiwa Tanzania kupitia Vision 2025 inalenga kujenga jamii yenye usawa na kukuza uchumi,ni dhahiri kwamba hii itafanikisha sana kukiwa na usawa kijinsia na haki ya kila mtu kulindwa,pia kila raia kujenga utu na kumlinda raia mwenzake kutoka kwenye kunyanyasika kijinsia. Mimi nitaanza kwa kuhamasisha katika wilaya ya Temeke nikiwa na ndoto kubwa ya kufikia nchi nzima hasa maeneo ambayo unyanyasaji wa kijinsia umekithiri.Jamii yako ni kioo chako jitazame kwa kupinga ukatili wa Kijinsia. Mungu ibariki Tanzania.

Khanga Tagline

Staha yangu heshima yako

Attachments

Comments