Challenge:

Khanga Design Challenge

FAMILIA YANGU FURAHA YANGU

ANTONIA HERMAN NSIMBI


Title

FAMILIA YANGU FURAHA YANGU

Name: Artist/Group

ANTONIA HERMAN NSIMBI

Describe your idea (200 Words)

ELIMU YA UZAZI WA MPANGO BADO HAIJAWAFIKIA VIJANA WENGI SANA HASA TANZANIA, WENGI WAO HUDHANI LABDA MATUMIZI YA DAWA NA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO NI KWA AJILI YA WATU WALIOKWISHA ZAA AU MALAYA LAKINI SIO KWELI NJIA HIZI NI NZURI KWA RIKA ZOTE YAANI VIJANA NA WATU WAZIMA AMBAZO WANAOSHIRIKI NGONO ILA KWA SASA HAWAKO TAYARI KUPATA MTOTO, KUNA NJIA NYINGI UKITAKA KUPANGA UZAZI KAMA VITANZI,VIJITI, KONDOM,KUTUMIA KALENDA,VIDONGE,SINDANO,UPASUAJI WA KUFUNGA MIRIJA NA KADHALIKA, NA FAMILI NYINGI WALIOTUMIA UZAZI WA MPANGO WANASEMA HAWAJUTII KUTUMIA NJIA HIZO. UTAFITI ULIOFANYWA NA SHUGHULI ZA KITAKWIMU KUTOKA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) IRENIUS RUYOBYA AMESEMA KWA MUJIBU WA UTAFITI WA AFYA YA UZAZI NA MTOTO NA VIASHIRIA VYA MALARIA WA MWAKA 2015/2016 AMESEMA TAKRIBANI WANAWAKE 4 KATI YA 10 WALIOOLEWA AMBAO NI SAWA NA 38% WANATUMIA NJIA YOYOTE YA UZAZI WA MPANGO, 32% YA WANAWAKE WANATUMIA NJIA YA KISASA, 6% WANATUMIA NJIA ZA ASILI, 13% WANATUMIA SINDANO, 7% WANATUMIA VIPANDIKIZI NA 6% WANATUMIA VIDONGE. KUTOTUMIKA KWA NJIA HIZI KUMESABABISHWA KUZALIWA KWA WATOTO WENGI AMBAO HAWAKUPANGWA, KUJIUA KWA WASICHANA KUKWEPA AIBU NA UTOAJI WA MIMBA WA MARA KWA MARA. WIZARA YA AFYA ITAENDELEA KUHIMIZA WANANCHI KUTUMIA UZAZI WA MPANGO ILI KUFANIKISHA AZMA YA SERIKALI KATIKA KUHAKIKISHA TANZANIA INAKUA NA WANANCHI WENYE AFYA BORA. KWA AJILI YA AFYA YA MAMA PAMOJA NA MTOTO, MIMBA ZINATAKIWA ZIACHANE KWA ANGALAU MIAKA MIWILI, WANAWAKE NI LAZIMA WASHAURIWE KUHUSU UCHAGUZI WA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO AMBAZO ZIPO KWA AJILI YAO. WANAWAKE WOTE WANATAKIWA KUPATIWA USHAURI NASAA JUU YA UZAZI WA MPANGO WAKATI WA UJAUZITO NA BAADA YA KUJIFUNGUA.

Khanga Tagline

TUTAITUNZA AHADI,UTAMU NI FAIDA

Comments