Challenge:

Khanga Design Challenge

Ya nini kunikatili!

Mariam Hassan Chizenga


Title

Ya nini kunikatili!

Name: Artist/Group

Mariam Hassan Chizenga

Describe your idea (200 Words)

Ubakaji ni tatizo kubwa katika jamii yetu na dunia kwa ujumla. Mabinti wamekuwa wakinyanyaswa na kukatiliwa kila siku imma na ndugu zao wakaribu au watu baki. Wakazi wa Temeke pia ni wahanga wa tatizo hilo. Kutoka chanzo cha data zilizokusanywa na TDHS za mwaka 2017 zinazohusu vitendo vya ubakaji vilivyoripotiwa, zinaonyesha kuwa asilimia 80% ya mabinti wa temeke wenye umri kati ya 0-14 ni wahanga wa janga hili ambapo katika kila kundi la mabinti watano wanne wamekatiliwa. Vitendo hivi vimekuwa vikizima ndoto za wengi kimasomo, kijamii pia. Machungu yake yamekuwa yakutosemeka kwani hayaelezeki kadri ya siku zinavyokwenda binti huyu anaishi na kukua nayo. Mabinti hawa Wa Temeke wamekuwa wakiambukizwa magonjwa ya zinaa na wengine hadi kupelekea vifo vyao, vitendo hivi vya kinyama vimepelekea kuwatafuna na kuwaharibu kisaikolojia siku hadi siku. Serekali imekua ikiongeza juhudi za kupambana na matendo haya mno ingawa baadhi ya familia hushidwa kutoa taarifa kwa kuogopea fedheha. Mabinti wengi wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na matatizo haya.Ili tuweze kutokomeza haya lazima jamii ishirikiane na serekali kwa kutoa taarifa na kutoa elimu katika jamii nzima, na wahusika wa haya wachukuliwe hatua kali. Kwani "Hata wao wanandoto pia, nimepoteza marafiki na thamani kwani huenda mimi ni kati yao."

Khanga Tagline

Ni nani wakunilipa thamani ya chozi langu?

Comments