Challenge:

Khanga Design Challenge

TUNAWAPA FUNZO GANI

michael michael


Title

TUNAWAPA FUNZO GANI

Name: Artist/Group

Michael C. Michael

Describe your idea (200 Words)

Ukatili wa kihisia kwa lugha ya kitaalamu (Emotional Violence). Ni tatizo linalowakumba watoto/vijana wengi hasa wa kike. Kutokana na takwimu za Wilaya ya Temeke mwaka 2017 zilizotolewa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, zinaonyesha kua kati ya watoto 10 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 19 wapo 3 walioathiriwa kijinasi. Tatizo hili husababishwa haswa na wazazi wenyewe hususani pale wanapojibizana na kugombana mbele ya watoto hii huleta funzo baya na kuwaathiri kihisia . hii pia hupoteza hamu ya watoto kukaa nyumbani. Katika kazi hii ya kisanii inaonesha jinsi tatizo hili la ukatili huu wakihisia chanzo chake ni familia hasa wazazi , hii imewakilishwa na umbo la kopa lenye vivuli viwili [cha mwanaume na mwanamke kama wazazi] na kopa mbili za pembeni zilizo beba takwimu ya tatu ya kumi [kuwakilisha watoto watatu kati ya kumi wathirika wa tatizo hilo]. Namba tatu hiyo yenye nyufa kuwakilisha mioyo ilio athiriwa na vitendo vya wazazi wao au walezi. Nje ya mji kuna kopa ambazo ziko kama mikono iliyo shikana kuwakilisha jinsi upendo unavyotakiwa kuwa . Na kama maneno ya khanga yasemavyo 'NIPENDE WAIGE' ndivyo wazazi wanatakiwa kuwa ili watoto wao wapate funzo zuri na wawaepushe kuwaathili watoto kihisia.

Khanga Tagline

NIPENDE WAIGE

Comments