Challenge:

Khanga Design Challenge

VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Gerald Mwita


Title

VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Name: Artist/Group

GERALD MWITA

Describe your idea (200 Words)

Takwimu kwa mwaka 2015/16 inaonesha kuna vifo 556 vya uzazi katika kila uzazi hai 100,000. Vifo hivi vinasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo kuzaa katika umri mdogo na ukosefu wa huduma za afya zenye kiwango kinachostahili kimataifa, vifaa tiba na utoaji holela wa mimba. Khanga hii imeweza kuonesha umuhimu wa kumlinda na kumsaidia mama na mtoto wake angali bado yupo tumboni. Kama inavooneshwa kwenye khanga jinsi mikono ilivoshikamana, ushirikiano wetu wenyewe kwa wenyewe unahitajika kuleta huduma za afya karibu na makazi, bila kutegemea serikali. Vilevile katika khanga hii, nimetumia mbegu kubwa na mbegu ndogo kuashiria mama na mtoto; mbegu kubwa ikiwa ni mama na mbegu ndogo ikiwa ni mtoto. Mama anazaa mtoto na mtoto akikua pia analeta mtoto na hao watoto ndo wanaunda taifa letu. Hivyo basi, ni jukumu letu sote kuhakikisha tunapambana kupunguza vifo vya mama na mtoto. Kama nilivyotumia rangi nyekundu kuashiria upendo, khanga hii ni ujumbe kwa jamii ya kwamba tupendane na tushikamane katika kulinda taifa letu.

Khanga Tagline

UZAO WANGU TAIFA LETU

Comments