Challenge:

Khanga Design Challenge

Nitendee wema nami na haki zangu

Nasry Ally


Title

Nitendee wema nami na haki zangu

Name: Artist/Group

Nasry Ally

Describe your idea (200 Words)

Wazo langu lakubuni hiki kitenge limetokana na unyanyasaji wa kijinsia katika wilaya ya temeke hasa kwa wanawake na watoto. Hili suala limeonekana kuwa kuwanyima raha wanawake na watoto wao pale wanapo dhulumiwa haki zao za msingi. “Nitendee wema na mie na haki zangu” ni design itakayo piga vita unyanyasaji thidi ya wanawake na watoto. Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF ‘Watoto na Wanawake Tanzania’ ya mwaka 2010 inasema kuwa kuwekeza kwa watoto na wanawake ni moja ya njia bora kabisa kwa maendeleo ya Tanzania. Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 inaonesha Zaidi ya asilimia 50 ni watoto, ubunifu wao na umahiri wao katika kuzalisha ndio msingi mkubwa wa kufikia malengo ya Tanzania 2025. Ripoti ya “Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania” ya UNICEF 2011, inasema kuwa karibu wasichana 3 kati ya 10 na mvulana 1 kati ya 7 wameripoti kutendewa walau tukio moja la ukatiliwa kijinsia kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Huku karibu asilimia 6 ya wasichana wamelazimishwa kujamiiana kabla hawajatimiza miaka 18. Marafiki, majirani, na watu wasiowafahamu walitajwa na wasichana na wavulana kama wakosaji wa ukatili wa kijinsia.

Khanga Tagline

nitendee wema

Comments