Challenge:

Khanga Design Challenge

Uharibifu wa Nguvu Kazi Basi

Sophia Erick Mwaikambo


Title

Uharibifu wa Nguvu Kazi Basi

Name: Artist/Group

Sophia Mwaikambo

Describe your idea (200 Words)

Ukatili wa kijinsia una dhoofisha maendeleo hasa kwa jamii husika pia matatizo kama vifo ulemavu wakudumu na kuharibika kisaikolojia. Hii ni mada inayogusa watu wengi katika jamii kutokana na ongezeko la matukio ya ukatili wakijinsia ni muhimu kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kwan wasichana wakike Chin ya miaka 18 ndio nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla. Mtungi mitatu katika Sanaa hii yakanga inawakilisha wasichana watatu ambao kila kwenye wasichana watatu mmoja amefanyiwa ukatili wa kijinsia kama ilivyoonyeshwa katika ufafiti wa TDHS,2010, (Tanzania Demographic Health Survey). Pia Sanaa hii imeonyesha tafiti hii kwa jinsi ya maua yenye duara tatu katk jamii ambapo duara moja imeharibiwa inakivul. Pia maneno ya Sanaa hii USINIHARIBU UTAIHARIBU JAMII ni sauti toka kwa mtoto wakike katika wilaya ya temeke akisisitiza kutofanyiwa ukatili ili atimize ndoto yake na aje kuisaidia jamii Ni wakati wa kila mtu kujua na kutambua wajibu wa kumlinda mtoto wa kike na kumthamini pia kumuwezesha afikie malengo yake ili kuja kuikomboa jamii husika.

Khanga Tagline

Usiniharibu Utaiharibu Jamii

Comments