Challenge:

Khanga Design Challenge

PAZA SAUTI TUTOKOMEZE UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Fred Halla


Title

PAZA SAUTI TUTOKOMEZE UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Name: Artist/Group

Fred Halla

Describe your idea (200 Words)

Ili Kupunguza na hatimaye kutokomeza kabisa Unyanyasaji wa kijinsia yatupasa KUPAZA SAUTI KUKEMEA na KULAANI vitendo hivyo kwa kupaza sauti pale inapotokea kuna dalili ama kumefanyika ukatili wa kijinsia. Alama ya mikono miwili; wenye rangi nyekundu inaonyesha kupinga/kuzuia ukatili wa kijinsia (ACHA ‘stop’) na mkono wa pili wenye rangi ya chungwa (Orange) unaonyesha kuelekea chini, maana yake kuondoa kabisa unyanyasaji na ikiwezekana kushusha takwimu kufikia sifuri.( Bila unyanyasaji tunaishi). Urembo huo wenye alama ya mihimili nje ya duara kuu ni alama ya takwimu ikionyesha kuwa Unyanyasaji uko katika kiwango cha juu na tunaweza kupunguza ama kutokomeza kabisa . Katika kuonyesha msisitizo wa kuwa na jamii isiyo na uyanyasaji wa kijinsia, kuna alama ya sifuri katika kingo kuzunguka Khanga pande zote nne za Khanga.

Khanga Tagline

PAZA SAUTI BAADAYE KITAELEWEKA

Comments